CAKE RAHISI :
hamna asiye fahamu utamu wa keki iliyo pikwa vizuri ikapikika. hii hapa receip rahisi sana ya kutengeneza keki.MAHITAJI KWA AJILI YA KUPIKA KEKI
-Siagi kikombe 1-Sukari kikombe 1
-Mayai 4
-Baking powder kijiko cha chai 1
-Unga wa ngano kikombe 1 na nusu
-Vanilla kijiko 1
JINSI YA KUANDAA KEKI YAKO
1.Kwenye bakuli tia Unga wa ngano na baking powder changanya vizuri kwa kijiko weka pembeni2.Washa oven 180c kama unapikia mkaa koleza jiko kabisa.
3.Saga siagi na sukari mpaka iwe laini, tia yai moja moja huku uwe unasaga vizuri mpaka mayai yamalizike , tia vanila changanya tena vizuri,
4.Tia unga wa ngano , saga kidogo tu malizia kukoroga na mwiko.
Paka mafuta kwenye trey chini ili cake isigande , tia mchanganyiko wako ueneze vizuri na ubake mpaka iwive, ichome na kijiti, kujiti kikitoka kikavu cake imewiva itoe, iwache ipoe kwa dakika 10 mpaka 15.
Kama unapikia kwenye mkaa weka moto juu na chini kama moto wa kupalilia wali.
5.Ikate kate vipande saiz unayotaka,kula na juice,chai n.k ENJOY.