Notification texts go here Contact Us Buy Now!
Machapisho

JE, UNAMFAHAMU MWANAMKE?

JE, UNAMFAHAMU MWANAMKE?
ZIJUE SIFA 13 ZA MWANAMKE

*DARASA LA MAHUSIANO*


Naomba msipanick walimu,
Ukinipinga pinga kwa hoja.

Wanawake ni binadamu wa ajabu sana katika uso huu wa Dunia yaani hawa watu ni next level, kuwaelewa ni ishu iliyowashinda hata wana falsafa, paulo na uwezo wake wote wa kufundisha hakuwahi kuwaelewa kabisa Wanawake. Mpaka anakufa aliishia kutuachia tu wosia wanaume kwamba "ISHINI NAO KWA AKILI (ndio maana haieleweki hata kama alioa).Sasa najiuliza ni jambo gani unaweza fanya bila kutumia akili?, hapa ndipo napata ushahidi kwamba kumbe wanawake walishindikana tangu zama za mwanzo kabisa!

Mara" simpi MWANAMKE ruhusa ya kufundisha" utadhani yeye ndiye aliwaumba😀😀😀 any way ni kwa kuwa hakuwahi kuwaelewa hawa viumbe.

 Wanasaikolojia wanasema kuwa kama utamuoa/kuishi na mwanamke  mwenye miaka 25 basi itakuchukua miaka 25 mingine kumuelewa huyo mwanamke angaalau kwa 90% maana hawa kila siku hubadilika na kuwa wapya kimatendo na kifikra.

1.Mwanamke unaweza mnunulia gari akatoka nayo kwenda kutembea, akiwa njiani akaombwa lift na kijana akampa akipitia sheli hela ya mafuta ikawa haitoshi, yule kijana akaamua kumuongeza ata elfu 20 basi mwanamke huweza kubadili mawazo na kumuona yule kijana ni bora kisa tu kachangia mafuta kuliko wewe uliyenunua gari, na akaamua kumtunuku yule kijana penzi.

2. Mwanamke unaweza mpa hela akanunue nyama kilo 5 buchani, mwenye bucha akimuongeza robo tu hilo litamfurahisha kiasi kwamba  anaweza kumpa mwenye bucha penzi na akusahau wewe ulieyota hela ya nyama kilo 5.

3. Mwanamke unaweza kumnunulia nguo, weaving, mafuta, perfume na urembo mzuri akavutia ila akipita mtaani akasifiwa na mwanaume kuwa kapendeza inaweza kuwa chanzo cha kumtunuku penzi na akakusahu wewe uliyegharamika na kufanya asifiwe

4.Mwanamke ndiye kiumbe pekee anayeweza kukupenda bila sababu ama kukuchukia bila sababu tofauti na viumbe wengine.

5. Mwanamke ndiye mwigizaji mkubwa ulimwenguni, anaweza kulia kama rose muhando kwa kupangwa tu.... Na MWANAMKE anaweza kulia kwa furaha na akacheka kwa huzuni, bado hujawajua tu wanawake!

6.Mwanamke akisema ndio humaanisha hapana, na akisema hapana humaanisha ndio, pia anaweza kucheka bila kujua sababu lakini pia anaweza kulia pasipo sababu ya msingi ya kumfanya alie, hivyo chunga sana usijejichanganya!.

7.Mwanamke hupenda vitu vigumu na vyenye hatari mfano wanaume wenye nguvu, muhuni (playboy), jambazi, mgomvi anayeogopwa hata na wanaume wenzie ila ukimuuliza anakwambia mie napenda kuwa na mwanaume mpole mwenye hofu ya Mungu tofauti na sisi wanaume tunavyopenda vitu vipole na vinyenyekevu na vyenye ukarimu, sasa wewe jifanye kumuamini mwanamke!

8.Jinsi unavyozidi kumpenda na kumthibutishia upendo wa dhati ndivyo unavyozidi kujiweka mbali nayeye, mwanamke hupenda migogoro isiyo na maana, ukijua hili ndoa haitokusumbua.

9. Mwanamke hapendi utulivu kamwe!, usipomchokoa atakuchokoa tuu na usipomuendesha lazima akuendeshe yeye, Hawa viumbe hawana hiyana aisee!.

10.Mwanamke hapendi vitu vikubwa wala vidogo, kiufupi hana chaguo maalumu. Ukimnunulia gari sio garantii ya yeye kutulia nawewe bali anaweza kukusaliti hata na muosha gari wako. Ukimjengea nyumba nzuri na kumuwekea kila kitu sio njia ya kumteka kimahaba kwani anaweza kumtunuku penzi ata mtunza bustani wa nyumba yako.

11.Mwanamke hapendi ukweli, Ukimpa ukweli akija mwenye uongo basi we  andika maumivu. Unaweza kuwa na elfu 5000 ukamueleza ukweli kuwa "mke wangu leo hali mbaya chukua hii elfu 30,"... akatokea jamaa akamuongopea kuwa "Chukua hii elfu 3000 ngoja nimesahau ATM card yangu nyumbani ikifuka saa 10 jioni  ntakutumia laki 2 kwenye simu", Usishangae mkeo akakusaliti hata kabla ya hiyo saa 10 na iyo laki 2 asiione katu!..   Tangu alipokubali kuingia kwenye mtego wa uongo toka kwa nyoka pale bustanini....MWANAMKE anapenda kudanganywa. Ndio maana kilio cha kila MWANAMKE ni "wanaume ni waongo"  ni kwa sababu wanaume wamewasoma wanawake hupenda kudanganywa.

12. Unaoa MWANAMKE unamwona ana karama ya kuimba anakuomba umpeleke aka record nyimbo zake...... Unamlipia keshi pesa ya album anafika studio produce anampa kaofa ka wimbo mmoja anampangia zamu ya usiku.... Basi utakuta anakusaliti kwa ofa tu ya wimbo mmoja utafikiri angekuomba usingemlipia.... anaamua kumsaliti maana wa Mungu aliyempa karama anamsaliti kwa kipande cha wimbo mmoja, halafu eti ana ndoto ya kuifikia tz imjue subutu!

13.Unamuoa hakuwa na ishu akiwa kwao amekaa tu,  unaamua kumfungulia biashara hata ya duka unamjazia kila kitu. anatokea jamaa mmoja kumuungisha pale dukani kila siku na kumuachia soda tu na hicho kinakuwa kigezo tosha cha kuona jamaa anamjali kwa kumuachia ya soda kila siku kuliko wewe uliyemfungulia duka zima na kinachofuata ni usaliti tu.

Mhubiri anasema ktk 7:28
Nilimtafuta,mwanamume mmoja katika elfu nimemwona; bali mwanamke mmoja miongoni mwa wote mimi sikumwona...... Yaani wote wanafanana tu.

Lakini MWANAMKE amchaye Bwana ndiye atakayesifiwa.

**

Maoni 1

  1. Hakuna jasiri👌SHUPAVU👌 mvumilivu👌mwenye nguvu, mbunifu, mwenye uwezo, mpambanaji na mchapakazi kama mwanamke👰mwanamke simama imara 👌 👌 acha kubweteka. Acheni ile kauli yakusema eti mwanamke akiwezeshwa anawezaa😀😀😀 hata sisi tunaweza kujiwezesha👌 usikae kusubiri nguvu yamtu ikutoe ulipo,👆kuolewa au kuzaa kusikufanye ukakosa haki zako zamsingi👌 simama sasa na uuvae ujasiri. Ukisimama wewe mwenyewe hakuna wa kukukalisha chini tena👌👌 MWANAMKE ❤️ SHUPAVU 🙏🙏🙏🙏
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.