Notification texts go here Contact Us Buy Now!

MOYO USINIDANGANYE SEHEMU YA 02

MOYO USINIDANGANYE 2


Endelea

Mwaka mzima ulipita, na wa pili, nikiwa singo kama wanavyosema vijana wa mjini. Biashara zilichanganya, kuna wakati nilipigwa, yaani niliibiwa kidogo na vijana wangu, lakini si kiasi cha kunitia hasara. Niliongeza mtandao, na marafiki katika biashara, kwani nilianza kuwa mkombozi katika upatikanaji wa nguo za ndani kwa urahisi na kwa bei nafuu pale Zanzibar. Baada ya muda nilikutana na binti mwingine, tukaanza mazoea na kuwa kama wapenzi. Nadhani nilichoshwa na upweke na kuamua kuwa kwenye mahusiano, japo sikuwa nimemaanisha sana. Mungu anisamehe, kwani mpaka leo nahisi sikumtendea haki yule mpenzi wangu mwingine baada ya Fatmah. Utanielewa baadaye.

Miezi michache tena ikapita, nikiendelea na biashara zangu na uhusiano wangu wa kupotezea muda. Nakumbuka siku moja, nikiwa Dar es Salaam, nikisubiri safari yangu kufata mzigo Uganda, siku moja kabla ya safari. Nikiwa kwa rafiki yangu Obey, tunakula chakula cha mchana kilichoandaliwa na mkewe  Obey alipigiwa simu na jamaa yake fulani akimualika kwa chakula cha jioni. Ni rafiki yake, walisoma naye miaka sita ya sekondari, waliishi naye chumba kimoja, kwa wakati huo walikuwa wamepotezana kama miaka miwili huku huyo jamaa akiwa jeshini ambako hakutakiwa kuwa na mawasiliano na watu. Alipopokea simu, alipata msisimko na hakutaka kutakaa kabisa ule mualiko. Alianza kutushawishi mimi na mkewe twende naye, lakini mke wake aliyekuwa na mimba changa hakutaka kusumbuka kabisa. Nilitaka kumkatalia pia, ili nijiandae na safari kesho yake, lakini alinishawishi sana, nikashindwa. Tukamuacha mkewe, na binti wa kazi, tukaondoka.

Tulikutana hoteli moja nzuri mjini Dar es Salaam, maeneo ya Posta, inaitwa lamada. Tulifika, na kuongoza kwenye meza moja yenye watu wawili, mwanaume na mwanamke, walioonekana ni wapenzi. Lahaula! Sikutaka kuamini macho yangu kile nilichoona mbele yangu. macho yangu yaligonga moja kwa moja katika sura ninayoifahamu, ya binti aliyewahi kunivutia kuliko wanawake wote kabla. Msichana niliyemuota na kutamani kuwa naye kuliko mwanamke mwingine yeyote. Ghafla akili yangu ilihama, nikajihisi kuchanganyikiwa, nikatamani tungeipita ile meza, yani wasiwe ndio hao watu ambao tutakaa nao. Lakini nikiwa katika lindi la mawazo, nilijikuta tayari tumekaa kwenye meza hiyo hiyo, na muhudumu ameshafika kutusikiliza. Obey na rafiki yake walisalimiana kwa furaha, Obey akanitambulisha, huku nikiwa kama mtu aliyenyeshewa. Tukatambulishwa pia huyo mrembo, aliyeitwa Latiffa, ambaye jamaa alisema ni mkewe mtarajiwa. Rohoni nikajisemea,”bora ni mtarajiwa”, huku nikijipa matumaini kwa mbaali kwamba kama bado hawajaoana pengine bahati inaweza kunigeukia mimi.

INAENDELEA...

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.